Jumamosi 10 Oktoba 2026 - 19:15
Wanazuoni Kutoka Najaf Ashraf Watembelea Dar-ul-Muslimeen Dodoma

Hawza/ Taasisi ya Kiislamu ya Dar-ul-Muslimeen, iliyopo mkoani Dodoma, imepokea wageni maalumu kutoka Hawza Kashmiriyyah iliyoko katika mji mtakatifu wa Najaf al-Ashraf nchini Iraq, katika ziara iliyolenga kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali za kielimu, kidini na kijamii zinazotekelezwa na taasisi hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Katika ziara hiyo, wanazuoni hao mashuhuri kutoka Najaf al-Ashraf walipokelewa na uongozi wa Dar-ul-Muslimeen, ambao uliwapa fursa ya kufahamu kwa karibu shughuli na huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo kwa ajili ya jamii.

Aidha, wageni hao walitembelea zahanati ya Dar-ul-Muslimeen, inayotoa huduma za afya kwa jamii, pamoja na shule za chekechea, msingi na sekondari zinazoendeshwa na taasisi hiyo. Ziara hiyo iliwapa fursa ya kujionea juhudi zinazofanywa na Dar-ul-Muslimeen katika kuimarisha huduma za afya na elimu, sambamba na malezi ya kidini na kijamii.

Dar-ul-Muslimeen ni miongoni mwa taasisi zinazojishughulisha na utoaji wa huduma za kielimu na kijamii, zikilenga kuchangia maendeleo ya jamii kupitia elimu na huduma za msingi. Ziara ya wanazuoni hao kutoka Najaf al-Ashraf inaonesha pia umuhimu wa kutembeleana na kufahamiana baina ya taasisi za Hawza zilizopo katika maeneo mbalimbali.

Ziara hiyo imekuwa fursa muhimu kwa wageni hao kufahamu shughuli zinazofanywa na Taasisi ya Dar-ul-Muslimeen Dodoma, katika kuendeleza elimu na kutoa huduma kwa jamii.

Wanazuoni Kutoka Najaf Ashraf Watembelea Dar-ul-Muslimeen Dodoma

Wanazuoni Kutoka Najaf Ashraf Watembelea Dar-ul-Muslimeen Dodoma

Wanazuoni Kutoka Najaf Ashraf Watembelea Dar-ul-Muslimeen Dodoma

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha